Social Icons

Monday 23 June 2014

Wanajeshi wa Amisom Watoa Kichapo Kwa Kundi la Kigaidi la Al Shabaab Huko Somalia


Wanajeshi wa Kenya walio chini ya Muungano wa Afrika, wameshambulia kambi za wapiganaji wa al Ahabaab huku idadi kubwa ya wapiganaji hao wakiuawa.



Taarifa hii ni kwa mujibu wa jeshi la Muungano wa Afrika nchini Somalia.Wanajeshi hao walianzisha operesheni yao mwezi Machi katika juhudi zao za kukomboa miji ambayo bado imetekwa na wapiganajihao.Mashambulizi ya angani yalifanywa na wanajeshi 22,000 wa Amisom, katika vijiji vya Anole na Kuday Kusini mwa eneo la Juba, nchini Somalia.
Wanajeshi wa Amisom, walifanya mashambulizi ya angani kama sehemu ya operesheni yao kuharibu uwezo wa kijeshi wa Al Shabaab.Kwa mujibu wa taarifa za wanajeshi hao, ndege za kivita za Kenya ndizo zilizofanya mashambulizi hayo.
Mashambulizi dhidi ya Al Shabaab yanakuja wiki moja baada ya Al-Shabaab kukiri mashambulizi mawili yaliyowaua watu sitini , ingawa serikali ililaumu wanasiasa kwa kuchochea mauaji hayo.Al Shabaab ilikiri kufanya mashambulizi hayo kama hatua ya kulipiza kisasi kwa wanajeshi wa Kenya kuwepo Kusini mwa Somalia, kama sehemu ya operesheni ya Amisom.
AU imesema kuwa mashambulizi ya angani yaliyofanywa katika eneo la Anole, yaliwaua wapiganaji 30 wa Al shabaab huku wengine 50 wakiuawa katika eneo la Kuday.Hata hivyo bado ni vigumu kuthibitisha idadi kamili ya wanjeshi waliouawa katika mashambulizi hayo.

No comments:

Post a Comment