Social Icons

Sunday 22 June 2014

Taarifa Kuhusu Wapiganaji wa Jihad Kuiteka miji zaidi Iraq Ipo Hapa


Wapiganaji wa Jihadi wameendelea kuyateka maeneo zaidi nchini Iraq,baada ya kuliteka eneo moja la kivuko karibu na mpaka wa Syria, na sasa wanalekea mjini Baghdad kupitia bonde la Euphrates.



Hatua hiyo inawafungulia njia wapiganaji wengine wa ISIS nchini Syria.Wapiganaji hao vilevile wameiteka miji zaidi katika mkoa wa Anbar ambapo mwandishi huyo anasema kuwa lengo lao ni kuitumia kuvamia mji mkuu wa Baghdad.

Waasi hao wanasema kuwa waliiteka miji hiyo bila kumwaga damu kupitia majadiliano na makabila ya kisunni.Wanamgambo wa Kishia hapo jana walifanya gwaride mjini Baghdad, na kuzua wasiwasi kuhusu tofauti inayozidi kuibuka kati ya watu wa dhehebu la kishia na wale wa Kisunni.

Source | BBC Swahili

No comments:

Post a Comment