Social Icons

Sunday 22 June 2014

Kutoka Kenya Watu 20 wameuawa katika shambulio kwenye kijiji Mashariki Kaskazini mwa Nchi Hiyo


Kuna taarifa kuwa watu ishirini wameuawa katika shambulio kwenye kijiji Mashariki Kaskazini mwa Kenya. Watu wenye silaha walivamia kijiji cha Gunana katika County ya Wajir mapema siku ya jumapili .Amesema mapigano yalizuka kutoka na mgogoro baina ya koo mbili za Degodia na Gare.


Ni mzozo wa mpaka baina ya koo hizo ambao wakuu wanautambua, lakini bado hawakuweza kuupatia ufumbuzi. Pamoja na kwamba kuliwahi kutokea mapigano mengine hapo awali lakini hayajawahi kusababisha vifo vya watu wengi kwa mara moja kama ilivyotokea siku ya jumapili.

 Moja ya mashambulizi ya kigaidi yaliyowahi kutokea nchini Kenya na kusababisha maafa

Mauaji haya yanakuja wiki moja baada ya watu wapatao 60 kuuwawa katika mashambulizi mawili yaliyotokea eneo la Mpeketoni katika pwani ya Kenya lililodaiwa kufanywa na wapiganaji wa Al Shabaab .Wapiganaji hao walivamia vijiji viwili karibu na mji wa Mpeketoni, na kufanya mashambulizi ambapo katika la kwanza lilisababisha mauaji ya wau 48 na baadae la pili liliua watu wapatao 20.

Source | BBC Swahili

No comments:

Post a Comment