Social Icons

Saturday 28 June 2014

Manchester United Yamnasa Luke Shaw Asaini Miaka 4, Adam Lallana Kupimwa Afya Liverpool , Barcelona Bado Inamtaka Suarez Aliefungiwa!!!


Wakati Manchester United ikimsaini Fulbeki wa England Luke Shaw na Liverpool ikiwa kwenye harakati za kumpima afya Kiungo wa England Adam Lallana, Barcelona ya Spain bado inaazimia kumnunua ‘Mfungwa’ Luis Suarez kutoka Liverpool.


Shaw asaini United
Manchester United wametangaza kukamilisha Uhamisho wa Fulbeki wa Southampton anaechezea England, Luke Shaw, kwa Mkataba wa Minne ambao unaweza kuongezwa Mwaka Mmoja.Shaw, mwenye Miaka 18, aliichezea England huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia ambako walitolewa Hatua ya Makundi lakini aliweka Rekodi ya kuwa Mchezaji mdogo kabisa kucheza Fainali hizo.
 

Shaw ameichezea Southampton Mechi 67 tangu alipoanza kucheza Mwaka 2012.Akiongelea Uhamisho wake, Shaw alisema: “Nimefurahishwa mno kujiunga na Manchester United! Nilikuwa Southampton tangu nina Miaka 8 na ningependa kuwashukuru pamoja na Mashabiki wote.”
 

Nae Meneja Msaidizi wa Manchester United assistant Ryan Giggs amesema: "Luke ni Fulbeki Kijana mwenye Kipaji sana na ana uwezo wa kuwa bora zaidi. Nimefurahi amejiunga na Manchester United!’’

Barcelona bado inamtaka Suarez aliefungiwa!

SUAREZ-AMNGATA-IVANOVIC 

Barcelona bado ina nia ya kumnunua Luis Suarez licha ya Mchezaji huyo wa Uruguay na Liverpool kufungiwa na FIFA Miezi Minne kwa kumng’ata Beki wa Italy Giorgio Chiellini kwenye Mechi ya Kombe la Dunia huko Brazil.Straika huyo mwenye Miaka 27 haruhusiwi kushiriki kwenye shughuli yeyote ya Soka mpaka mwishoni mwa Oktoba.

Kifungo hicho ni pamoja na kuzuiwa kufanya Mazoezi na Klabu yake na pia kuingia Uwanja wowote wa Soka kwenye kipindi hicho.Hata hivyo, habari kutoka ndani ya Barcelona, ambayo inao Masupastaa Lionel Messi toka Argentina na Neymar wa Brazil, zimedai Klabu hiyo iko tayari kumchukua Suarez ikiwa Dau ni muafaka.
 

Liverpool ilimnunua Suarez kutoka Ajax Mwaka 2011 kwa Pauni Milioni 25.
Mwaka Jana, Suarez alizikosa Mechi 10 baada ya kufungiwa kwa kumng’ata Meno Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Mwezi Aprili na kuukosa mwanzo wa Msimu uliopita lakini alirejea Uwanjani na kufunga Bao 31 wakati Liverpool inamaliza Nafasi ya Pili.
 
Uchezaji wake Msimu huo ulimfanya ashinde Tuzo za Mchezaji Bora wa Mwaka zilizotolewa na Wanahabari na ile ya Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa, PFA.

Adam Lallana kupimwa afya Liverpool
Kiungo wa Southampton Adam Lallana anatarajiwa kupimwa afya yake Klabuni Liverpool ili kukamilisha Uhamisho wa kwa Dau la Pauni Milioni 25.Liverpool walipeleka Ofa mbili huko Southampton na zote kukataliwa na sasa inaonekana mambo yamenyooka.
 

Lallana atakuwa Mchezaji wa Pili wa Southampton kujiunga na Liverpool kwa ajili ya Msimu mpya na anamfuatia Rickie Lambert alienunuliwa kwa Pauni Milioni 4.Vile vile, Southampton imemuuza Fulbeki wao Luke Shaw kwa Manchester United.
 

Mbali ya Lallana na Lambert, Liverpool tayari pia imekubaliana na Bayer Leverkusen ili Kiungo Emre Can ajiunge Anfield kuanzia Julai Mosi.

No comments:

Post a Comment