Social Icons

Thursday 26 June 2014

Ni Rasmi Kiungo wa Athletic Club Bilbao Ander Herrera Asaini Manchester United


Mabingwa wa zamani wa England Manchester United Leo hii wametangaza kuwa Kiungo kutoka Spain Ander Herrera amesainiwa Klabuni hapo kutoka Athletic Club ya Bilbao.

Herrera, mwenye Miaka 24, amesaini Mkataba wa Miaka Minne kukiwa na Kipengele cha Nyongeza ya Mwaka mmoja zaidi.

Kiungo huyo, ambae sasa anasubiri Shahada ya Kimataifa ya Uhamisho ilikuubariki kikamilifu Uhamisho huu, alijiunga na Bilbao Mwaka 2011 akitokea Real Zaragoza na kuichezea Mechi 128 na kufunga Bao 11.

Pia amezichezea Timu za Taifa za Vijana za Spain za chini ya Miaka 20, U-20, na pia U-21 na U-23.Mchezaji huyo anakuwa wa kwanza kusainiwa chini ya Meneja mpya Louis van Gaal ambae sasa yuko huko Brazil kama Kocha wa Netherlands.


Akimpokea Mchezaji huyo mpya, Meneja Msaidizi wa Man United, Ryan Giggs, alisema: “Ander ni Kijana mdogo hodari mwenye nguvu na ubunifu. Tunaamini yeye ni Chipukizi atakaeng’ara sana huko Spain na nina hakika atapendwa na Mashabiki wetu. Nimefurahi ameichagua Manchester United. Nangojea kwa hamu tuwe nae kwenye Ziara ya kabla Msimu mpya huko Marekani.”

Nae Ander Herrera amesema: “Kusaini Manchester United ni ndoto iliyotimia. Nimecheza Old Trafford na Athletic Club kwa Mechi za Ulaya na hiyo ni kumbukumbu kubwa kwangu. Nimejiunga ili kuisaidia Klabu kutimiza malengo yake yote. Ninafuraha sasa kuishi Jijini Manchester na nangojea kwa hamu nivae Jezi Nyekundu inayosifika ya United. Sitasahau muda wangu na Athletic Club na nataka niwashkuru Mashabiki wote na Wafanyakazi kwa sapoti yao na juu ya yote nawashkuru Wachezaji wenzangu wa zamani na kuwatakia kila la heri hapo baadae.”

No comments:

Post a Comment