Social Icons

Thursday 26 June 2014

ANDER HERRERA Kununua Makataba wake ili kulazimisha Uhamisho wake kwenda Manchester United


ANDER HERRERA ataununua Makataba wake na Klabu ya Athletic Bilbao ili kulazimisha Uhamisho wake kwenda Manchester United baada ya Klabu hiyo ya Spain kukataa kumuuza.

 
Ingawa Man United walitimiza Kipengele cha Mkataba wa Herrera kinachotaka ilipwe Pauni Milioni 29 ikiwa atataka kuhama kabla Mkataba haujamaliziki, Bilbao Leo imetangaza kuikataa Ofa hiyo.

Imedokezwa sasa njia pekee ni kwa Man United kumpa Fedha hizo Herrera ili aununue Mkataba wake na kuwa Mchezaji huru na kisha kuhamia Old Trafford.Sakata kama hili lilitokea Miaka miwili iliyopita wakati Javi Martinez alipotaka kuihama Bilbao na kuhamia Bayern Munich na kugomewa.Mchezaji huyo alilazimika kuununua Mkataba wake na kisha kuhamia Bayern kama Mchezaji huru. 

Wachambuzi wanasema hii ni mbinu spesho ya Bilbao ili wasichefue Washabiki wao na kuoneka wako tayari kuuza Wachezaji bali husukuma lawama kwa Wachezaji ili waonekane wao ndio wamelazimisha Uhamisho.Habari za ndani toka Old Trafford zimedokeza kuwa wana imani Uhamisho huu utakamilika muda si mrefu hasa baada ya Jana Herrera, mwenye Miaka 24, kupasi upimwaji afya na kukubali Mkataba wa Miaka minne na Man United huku Picha maalum zikiwa tayari zimepigwa na Mchezaji huyo pia kurekodiwa na MUTV, Stesheni ya TV ya Man United.Herrera anatarajiwa kuwa Mchezaji wa kwanza kusainiwa na Meneja mpya Louis Van Gaal.

MANCHESTER CITY YAMSAINI KIUNGO WA FC PORTO FERNANDO
Manchester City imekamilisha Uhamisho wa Kiungo kutoka Brazil Fernando anaechezea FC Porto ya Ureno.Habari hizi zimetangazwa na FC Porto na kusema Uhamisho wake ni kwa Dau la Pauni Milioni 12. 

Fernando anakuwa Mchezaji wa pili kusainiwa na Man City kwa ajili ya Msimu mpya na mwingine ni Bacary Sagna aliekuwa Arsenal.Fernando alijiunga na FC Porto Mwaka 2007 na kutwaa Ubingwa wa Ureno mara 4 na EUROPA LIGI Mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment