Social Icons

Friday 20 June 2014

Roy Hodgson amesema hana nia ya kujiuzulu licha ya Timu yake kuchungulia kutupwa nje Kombe la Dunia


MENEJA wa England Roy Hodgson amesema hana nia ya kujiuzulu licha ya Timu yake kuchungulia kutupwa nje baada ya kufungwa Mechi yao ya Pili ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.Jana, Bao 2 za Luis Suarez, anaecheza Liverpool, ziliwaua England Bao 2-1 katika Mechi yao ya Pili ya Kundi D.

Kwenye Mechi ya Kwanza England walipigwa 2-1 na Italy.Wayne Rooney ndie aliefunga Bao la England na kufunga midomo ya Watu waliokuwa wakimpinga na sasa hao hao wakingojewa kusema kama watamnanga Steven Gerrard ambae ndie alitoa upenyo kwa mwenzake wa Liverpool Suarez kufunga Bao la ushindi.
Ikiwa Leo Italy na Costa Rica zitatoka Sare basi England wako nje lakini matokeo mengine yanawapa nafasi England ikiwa wataifunga Costa Rica kwenye Mechi ya mwisho na Matokeo mengine kwenda kwao.Lakini Meneja wa England, Roy Hodgson, amekata kujiuzulu na kuiacha FA iamue inachotaka.

KOMBE LA DUNIA
MSIMAMO
KUNDI D
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
Costa Rica
1
1
0
0
3
1
2
3
Italy
1
1
0
0
2
1
1
3
Uruguay
2
1
0
1
3
4
-1
3
England
2
0
0
2
2
3
-1
0

No comments:

Post a Comment