Social Icons

Monday 23 June 2014

Kocha Wa Timu Ya Taifa Ya Brazil Scolari Achukizwa na Madai Ya Kwamba Wanaweza Kuchagua Mpinzani Raundi Ijayo


Kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari, amekanusha kuwa Mechi yao ya Leo ya mwisho ya Kundi A na Cameroon itawanufaisha ili kupanga Mpinzani wao wa Raundi ya Pili ya Mtoano.Brazil wanahitaji Sare wakicheza na Cameroon ili kufuzu Raundi ya Pili na kabla ya Mechi hiyo,



wao watajua wazi nani atakuwa Mpinzani wao Raundi ijayo kwa vile Wapinzani wao watatoka Kundi B, na ni ama Netherlands au Chile, ambao watacheza Mechi yao ya mwisho kati yao mapema kabla Brazil v Cameroon.

Scolari amechukizwa na dhana hiyo ya ‘kupanga Mpinzani’ na kusema maneno hayo ni ‘upumbavu au yana nia mbaya.’Mapema Jana, Kocha wa Netherlands, Louis Van Gaal, aliilaumu FIFA kwa kupanga Mechi za Kundi A baada ya zile za Kundi B kumalizika.

FAHAMU:
-Mshindi wa Kwanza Kundi A atacheza na Mshindi wa Pili Kundi B
-Mshindi wa Kwanza Kundi B atacheza na Mshindi wa Pili Kundi A

Lakini Scolari ameponda fikra hizo kwamba Mechi yao na Cameroon itatawaliwa na nini kitatokea kwenye Mechi ya mapema ya Netherlands v Chile na kueleza hilo ni kuwavunjia heshima Wapinzani wao Cameroon.

Scolari amefoka: “Ni lazima tushinde. Watu wengine wanazungumza bila kuelewa hivi vitu, wanasema tutachagua Mpinzani! Ama ni wapumbavu au wana nia mbaya! FIFA ndio walipanga Ratiba na wametuweka kwenye hali ngumu, hii ni kuwavunjia heshima Cameroon na sipendi hili! Sina lazima kuchagua Mpinzani, inabidi nicheze na kushinda!

Kundi A Mechi za Mwisho:
-Croatia v Mexico
-Cameroon v Brazil
Brazil na Mexico zinahitaji Sare tu kufuzu.
Lakini Brazil inaweza kufuzu hata ikifungwa na Cameroon ikiwa Mexico itaifunga Croatia.Ili Croatia ifuzu inahitaji ushindi ingawa Sare inaweza kuwapitisha ikiwa tu Brazil itafungwa na Cameroon.

Kundi B Mechi za Mwisho:
-Australia v Spain
-Netherlands v Chile
Tayari Netherlands na Chile zimefuzu na Mechi kati yao itaamua nani Mshindi wa Kwanza wa Kundi.Netherlands wanahitaji Sare tu wabaki kileleni.

No comments:

Post a Comment