Social Icons

Monday 23 June 2014

Hii Ndio List Ya Wachezaji 11 Wa Yanga Waliotangazwa Kutovaa Uzi Wa Yanga Msimu Ujao, Itazame Hapa


Ikiwa dirisha la usajili limeshafunguliwa tangu wiki iliyopita kwa timu mbali mbali kuanza kufanya usajili wa wachezaji na zingine zikianza mazoezi, timu ya Young Africans imeweza kuweka wazi majina ya awali ya baadhi ya wachezaji ambao hawataitumikia katika msimu ujao wa 2014/2015.



Young Africans ambayo msimu uliopita ilikua na kikosi bora kabisa ambacho kiliweza kuwatoa jasho Mabingwa wa Kihistoria Barani Afrika timu ya Natioal Al Ahly katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika, ambapo Mabingwa hao wa kutoka nchini Misri waliweza kusonga mbele kwa mikwaju ya penati.
Msimu uliopita Young Africans ilikuwa na kikosi cha wachezaji 30 kutoka timu ya Wakubwa na wachezaji watano (5) kutoka timu ya vijana  (U20) waliokuwa wamepandishwa kwa ajili kupata uzoefu na kuingozea nguvu timu ya wakubwa katika michezo mbalimbali.
Kutokana na ripoti ya Benchi la Ufundi iliyowasilishwa mara baada ya kumalizika kwa Msimu wa Ligi Kuu 2013/2014 baadhi ya wachezaji hawataitumikia tena Yanga SC kwenye msimu ujao, wachezaji 11 wamemaliza muda wao na kumalizana na uongozi hivyo wapo huru kujiunga vilabu mbalimbali:
Wachezaji hao ni:
1. David Luhende
2. Athuman Idd “Chuji”
3. Geroge Banda -U20
4. Yusuph Abdul -U20
5. Rehani Kibingu -U20
6. Hamisi Thabiti
7. Reliants Lusajo
8. Bakari Masoud – U20
9. Shaban Kondo
10. Abdalllah Mguhi “Messi” U-20
11. Ibrahim Job
Hii ni orodha ya awali ya wachezaji ambao hawataitumikia Yanga SC msimu ujao, huku zoezi la usajili likiendelea kujaza baadhi ya nafasi zilizopo kulingana na maelekezo ya Benchi la Ufundi.

No comments:

Post a Comment