Social Icons

Saturday 21 June 2014

Taarifa Juu ya Kiongozi wa Muslim Brotherhood kunyongwa Ipo Hapa


Wakili mmoja nchini Misri amesema kwamba mahakama imezingatia hukumu ya kifo cha wanachama 182 wa kundi la Muslim Brotherhood .Washtakiwa hao ni miongoni mwa watu 700 wanaoshtakiwa kwa kukishambulia kituo kimoja cha polisi katika eneo la Minya mwaka uliopita.
kiongozi wa kundi hilo Mohammed Badie ni miongoni mwa wale waliohukumiwa kifo.Washtakiwa wengine watano walipewa hukumu nyengeine ya kati ya miaka 15 na 55 huku wengine wakiachiliwa huru.

           Wanachama wa kundi la MUslim Brotherhood wakiwa mahakamani

Hukumu iliotolewa mnamo mwezi Aprili ambapo jaji aliwapatia hukumu ya kifo washtakiwa wote ilizua pingamizi kutoka kwa makundi ya kupigania haki za kibinaadamu.

Source; BBC Swahili

No comments:

Post a Comment