Social Icons

Saturday 28 June 2014

Fifa Yatetea Adhabu Zake Ilizompa Straika wa Uruguay Luis Suarez (NG'ATA NG'ATA)


Fifa imetetea Adhabu zake ilizompa Straika wa Uruguay Luis Suarez kwa kumuuma Meno mpinzani Uwanjani lakini Nchi yake imekasirishwa na Kocha wao kuamua kujiuliza toka Jopo la Ufundi la FIFA.




Suarez amefungiwa na FIFA Miezi minne kutojihusisha na chochote kuhusu Soka ikiwemo kutokanyaga Mazoezi na kutoingia Uwanja wowote wa Mpira na pia kutocheza Mechi 9 za Kimataifa za Uruguay pamoja na kupigwa Faini ya Dola 111,000.

Lakini Uruguay imedai Mchezaji wao ameonewa na hilo limemfanya Kocha wao, Oscar Tabarez, kutangaza kujitoa Jopo la Ufundi la FIFA la Makocha kwa madai hawezi kushirikiana na Taasisi isiyokuwa na haki.Hata hivyo, Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, amesema Adhabu ya Suarez ni sahihi na imezingatia makosa yake ya Siku za nyuma. 

Suarez amewahi kufungiwa mara 2 kwa kosa hilo hilo la kung’ata Wachezaji wa Timu pinzani wakati wa Mechi.Jerome Valcke ameeleza: “Hii si mara ya kwanza na ilibidi tutoe fundisho. Tukio lile limeonekana na Mamilioni ya Watu Dunia nzima. Hilo halitakiwa kuonekana na Watoto Dunia nzima wanaocheza Soka.” 

Vile vile, Jerome Valcke amemtaka Suarez kutafuta ushauri wa Madaktari wa Saikolojia ili kumfanya asirudie tena kosa hilo.Kwenye Mahojiano na Wanahabri kuhusu Mechi yao inayowakabili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Kombe la Dunia dhidi ya Colombia, Kocha wa Uruguay, Oscar Tabarez, alikataa kuongea chochote na badala yake kusoma Taarifa ya Dakika 14. 

Kwenye Taarifa hiyo, Tabarez amevilaumu Vyombo vya Habari, na hasa vya Uingereza, kwa kuukuza mgogoro huo kutomtakia mema Mchezaji wao.Jana Ijumaa, Suarez alirudishwa Nchini kwao Uruguay. 

Mbali ya Adhabu, Suarez sasa pia anakabiliwa na kuachwa na Wadhamini ambapo wengine wameshamtoa kwenye udhamini huku Adidas ikitangaza kutomtumia katika Matangazo yao ya Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment