Social Icons

Thursday 26 June 2014

Taarifa Kuhusu Sulley Muntari na Kevin-Prince Boateng Kufukuzwa Katika Kikosi cha Timu ya Ghana huko Brazil


Sulley Muntari na Kevin-Prince Boateng wamefukuzwa kutoka Kikosi cha Timu ya Ghana kilichopo huko Brazil kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kutokana na ukosefu wa nidhamu.

 
Chama cha Soka cha Ghana, GFA, kimethibitisha kufukuzwa kwa Wachezaji hao na kusema pia wamesimamishwa kwa muda usiojulikana.Taarifa hiyo ya GFA ilifafanua kuwa Boateng alitumia ‘lugha chafu na ya matusi’ kwa Kocha Kwesi Appiah wakati Muntari alimshambulia na kumpiga Mjumbe wa Kamati Kuu. 

Inadaiwa tukio hilo la utovu wa nidhamu lilitokea Jumanne wakati Muntari alipomshambulia na kumpiga Moses Armah.Nae Boateng anadaiwa kutukana Siku hiyo hiyo Mazoezini na hakutaka hata kuomba samahani. 

Ghana, ambao Leo hii wanacheza na Portugal kwenye Mechi ya mwisho ya Kundi ambayo wanatakiwa kushinda huku Mechi ya Germany na USA iwapendelee, wamekuwa kwenye msukosuko huku Wachezaji wakidai Malipo yao.


Jana, Serikali ya Ghana ilikodisha Ndege kwenda Brazil kupeleka Dola Milioni 3 kuwalipa Wachezaji kwani walikuwa wametishia kugomea kucheza Mechi yao na Portugal.Ili kuingia Raundi ya Pili ya Mtoano Ghana ni lazima waifunge Portugal na kuombea Mechi ya Germany na USA itoe Mshindi wa Goli nyingi ili wao wapite kwa ubora wa tofauti ya Magoli ikiwezekana.

No comments:

Post a Comment