Social Icons

Saturday, 7 June 2014

Kuelekea Brazil Ujerumani yauwa 6 Mechi ya kirafiki, Wenyeji washinda 1 Dhidi ya serbia


Jana, kwenye Mechi ya Kirafiki huko Die Coface Arena, Jijini Mainz, Germany,Miroslav Klose aliweka Rekodi ya kuwa Mfungaji Bora wa Germany ambayo iliifunga Armenia Bao 6-1 lakini imekumbwa na wasiwasi baada kuumia Mchezaji wao Marco Reus.
Klose, mwenye Miaka 35, alitoka Benchi na kufunga Bao lake la 69 kwa Germany na kumfanya awe ndie Mfungaji Bora wao katika Historia.Andre Schurrle alitangulia kuipa Germany Bao na Armenia kusawazisha kwa Penati ya Henrik Mkhitaryan na hapo ndipo Germany iliposhusha Mvua ya Magoli.

MAGOLI
Germany 6
52' Andre Schurrle
72' Lukas Podolski
73' Benedikt Howedes
76' Miroslav Klose
82' Mario Goetze
89' Mario Goetze
Armenia 1
69' Henrik Mkhitaryan [Penati]

Baada ya Mechi, Kocha wa Germany, Joachim Low, aliongea: "Reus anachunguzwa Hospitali.  Tunasubiri. Mpaka Masaa 24 kabla ya Mechi ya Kwanza, kwa mujibu wa Sheria, tunaweza kumwita Mchezaji mwingine kumbadili!”

WENYEJI BRAZIL WAIPIGA SERBIA 1-0!

Pia jana,Wenyeji wa Mashindano ya FIFA ya kuwania Kombe la Dunia, Brazil, waliwafunga Serbia Bao 1-0 huko Arena de São Paulo, au kwa Jina jingine Arena Corinthians.Bao la Brazil lilifungwa katika Dakika ya 58 na Frederico Guedes Fred na kuwapa ushindi wao wa 15 katika Mechi 16 zilizopita.Hulk aliifungia Brazil Bao safi lakini Refa Enrique Cáceres alilikataa kimakosa kwa madai ya Ofsaidi.Alhamisi Brazil watacheza Mechi ya Ufunguzi ya Kombe la Dunia, wao wakiwa KUNDI A, dhidi ya Croatia.

VIKOSI:
Brazil
12 Julio César
02 Dani Alves (Maicon - 72')
06 Marcelo (Maxwell - 74')
17 Luiz Gustavo
03 Thiago Silva
04 David Luiz
07 Hulk
08 Paulinho (Fernandinho - 65')
09 Fred (Jô - 75' )
11 Oscar (Willian - 45')
10 Neymar (Bernard - 81')

Serbia
01 Stojkovic (Lukac - 89')
18 Basta (Vulicevic - 87')
11 Kolarov
14 Matic Booked
06 Ivanovic
03 Tosic
16 Jojic
08 Petrovic Booked (Mrdja - 86')
19 Mitrovic (Djordjevic - 80')
10 Tadic (Tosic - 70')
21 Markovic (Gudelj - 81')

No comments:

Post a Comment