1.Diamond alipokelewa kistaa na kama mastaa wengine wote walivyopokelewa ambapo meneja wake Bab Tale anasema ‘imefika sehemu unaona kabisa jamaa wanatukubali sasa hivi, Airport tumepokelewa na magari matatu… mi sijawahi kupokelewa na kuendeshwa na Mwanamke mzungu yani ila kiukweli Diamond amepokelewa kifahari kama wengine’
2.Babtale amethibitisha kwamba Diamond ndio atakua msanii wa kwanza kufungua show leo kweye utolewaji wa tuzo hizi ‘kitendo cha msanii kupewa nafasi ya kufungua, kwa sababu MTV ni kubwa…. kitendo hicho ni kikubwa kwa msanii pia‘
- ‘Wakati wa mazoezi tulikutana na Mafikizolo wasanii kutoka Afrika Kusini ambao wamekuja wenyewe kuomba kolabo na Diamond, wao wenyewe wanasema bwana tunaomba kolabo na wewe…….. sisi tulitakiwa kurudi bongo Jumapili lakini wao ndio wamesema watalipia gharama za sisi kuendelea kukaa hapa na mabadiliko ya ticket yetu ili turudi Tanzania Jumanne’ – Bab Tale
- ‘Hatukua tunajua kwamba Diamond ndio atafungua show kwenye utolewaji wa tuzo hizi za MTV, jana wakati tukiwa kwenye mazoezi ndio tukaambiwa’
-
‘Muziki unahitaji elimu na kujitambua, hata Mafikizolo walivyokuja
kwetu wanasema kabisa wanahitaji umoja wa Afrika wakati nyumbani bongo
tu yenyewe kwa wenyewe hawazimiani, Mafikizolo walivyofanya mkutano na
waandishi wa habari yani kwa jinsi walivyoelezea kuwa na ndoto ya
kufanya kolabo na Diamond….. imeonyesha ni jinsi gani Diamond ana nguvu’
– Bab Tale
-
Msimamizi mwingine wa Diamond ni meneja Mkubwa Fela ambae
amethibitisha kwamba kwenye safari yake ya kuja South Africa ameambatana
na Watanzania wengine saba ila kilichomfurahisha zaidi ni kwamba
amekuja kukuta washkaji zake zaidi ya 20 wanaoishi Durban wameshanunua
ticket tayari kwa ajili ya kumshangilia Diamond’
Watanzania waliofunga safari kutoka Tanzania mpaka Durban ni pamoja na Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Bab Tale, Salam ambae pia ni meneja wa Diamond, Mkubwa Fela, Watangazaji Sam Misago, B12, Adam Mchomvu, Millard Ayo, Shadee lakini pia Nancy Sumari na mpenzi wake Lucas, Ommy Dimpoz, Shetta na mpiga picha Michael Carter Mlingwa.
No comments:
Post a Comment