Kushiriki kwa Alex Oxlade-Chamberlain
kwenye Fainali za Kombe la Dunia zinazoanza Nchini Brazil Alhamisi Juni
12 kupo kwenye hati hati kubwa baada ya Kiungo huyo wa Arsenal kuumia
Goti kwenye Mechi ya Jumatano Usiku ambayo England walitoka 2-2 na
Ecuador huko Miami, Marekani.
Oxlade-Chamberlain, mwenye Miaka 20,
anaendelea kutibiwa na kuchunguzwa na Madaktari wa England lakini habari
za awali zimedai kuwa anahitaji Siku 10 hadi Wiki 3 ili apone.Ingawa Juni 2 ndio ilikuwa Siku ya
mwisho kwa Timu zote 32 zilizopo Fainali za Kombe la Dunia kuwasilisha
Listi yao ya Wachezaji 23, lakini Timu zinaweza kubadili Mchezaji hadi
Juni 13 ikiwa FIFA itaridhishwa kuwa mabadiliko hayo ni kwa ajili ya
Majeruhi tu.
WACHEZAJI 7 WA AKIBA:
-John Ruddy (Norwich)
-John Flanagan (Liverpool),
-John Stones (Everton),
-Michael Carrick (Man Utd),
-Jermain Defoe (Toronto),
-Andy Carroll (West Ham),
-Tom Cleverley (Man Utd).
Kocha wa England, Roy Hodgson, amekiri:
“Itakuwa pigo kubwa kumkosa. Alifanya vizuri sana kwenye Mechi na
alionekana kuwa mwepesi mno!”Mechi hiyo na Ecuador ilikuwa ni Mechi
ya kwanza ya Oxlade-Chamberlain tangu Aprili 20 alipoumia Nyonga akiwa
na Klabu yake Arsenal.jana, Oxlade-Chamberlain alikuwepo
Mazoezini huko Kambini kwa England, Barry University, Miami, akifanya
Mazoezi mapesi huku akiwa na Bendeji Gotini.
No comments:
Post a Comment