Social Icons

Friday 6 June 2014

Taarifa ya Amnesty International kuhusu Boko Haram


Shirika la Amnesty International linasema kuwa takriban watu 1500 wameuawa katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu Kaskazini mashariki mwa Nigeria katika mauaji yanayosemekana kufanywa na kundi la kiislamu la Boko Haram.Idadi hiyo iko juu zaidi ikilinganishwa na ilivyokadiriwa.
Wengi wa waathiriwa ni raia lakini wanamgambo hao pia wamezilenga taasisi za kijeshi pamoja na shule.
 Shirika la Amnesty International linasema kuwa watu 1500 wameuawa katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.Kadhalika Shirika hilo linaamini kuwa watu 600 waliuawa siku moja mapema mwezi huu baada ya wanamgambo kuvamia kambi moja ya kijeshi katika mji wa maiduguri na kuwaachilia wafungwa.

Jeshi la Nigeria linasema kuwa linapiga hatua katika harakati ya kuwafurusha wanamgambo wa Boko Haram katika maficho yao ya milimani karibu na mpaka na Cameroon.Lakini shirika la Amnesty International linasema kuwa vikosi vya usalama vya Nigeria pamoja na wanamgambo hao wa Boko Haram wanakiuka haki za kibinaadamu ikiwemo kutekeleza uhalifu wa kivita mbali na uhalifu dhidi ya binadaamu.Inasema kuwa maafa yanayotekelezwa na Boko haram ni ya kutamausha na kwamba yanasababisha hofu na ukosefu wa usalama.

No comments:

Post a Comment