Saturday, 7 June 2014
Mgomo wa Madereva Dala Dala Sio Bongo Pekee, Tazama hapa jinsi Madereva wa umma walivyogoma Brazil
Maafisa wa polisi nchini Brazil wametumia gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji katika siku ya pili ya mgomo wa wafanyikazi wa sekta ya uchukuzi ambao umesababisha uhaba mkubwa wa usafiri wa uma katika mji wa Sao Paulo.
Takriban nusu ya vituo vya treni vilifungwa na kusababisha msongamano mkubwa wa watu katika barabara za mji huo mkubwa ambao unatarajiwa kuandaa michuano ya kombe la dunia kuanzia alhamisi ijayo.
Wafanyakazi hao wa treni wanataka mishahara yao kuongezwa kwa asilimia kumi.Awamu nyengine ya majadiliano imefeli na wafanyikazi hao wanasema kuwa mgomo huo utaendelea kwa mda usiojulikana.
Labels:
AddyTz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment