Social Icons

Friday 6 June 2014

Kombe la Dunia-UTABIRI:Fainali ni BRAZIL v ARGENTINA, Bingwa BRAZIL


Fainali za kombe la dunia zinaanza Juni 12 huko Brazil, na kama ilivyo desturi kwa Mashindano makubwa ya aina hii, Watabiri hujitokeza kama ilivyokuwa Fainali za Mwaka 2010 ambako Pweza maarufu wa huko Ujerumani, aliebatizwa ‘Paulo Ze Pweza’,
alipopata umaarufu mkubwa kwa kutabiri kwa usahihi kabisa matokeo ya mechi za Soka za Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini.Lakini safari hii waliojitokeza na kutabiri kuwa Fainali ya Kombe hili hapo Julai 13 Uwanjani Maracana Jijini Rio de Janeiro itakuwa kati ya Wenyeji Brazil na Mahasimu wao wakubwa Argentina ni Benki ya Rasilimali ya Marekani, Goldman Sachs.


Goldman Sachs, kwenye Ripoti yao, wametathmini kuwa upo uwezekano wa Asilimia 48.5 kwa Brazil kushinda Fainali ya Julai 13 wakifuatiwa na Argentina, wenye Asilimia 14.1 na Germany, Asilimia 11.4.
Utabiri wa Benki hiyo umejengeka kwenye misingi ya kutathmini Mechi 14,000 za Kimataifa za Mashindano rasmi tangu Mwaka 1960.

Tathmini na Utabiri huo wa Goldman Sachs umeandikwa na Wachumi Wakuu Jan Hatzius, Sven Jari Stehn na Donnie Millar, ambao wamesema haishangazi kwa Brazil kupewa nafasi kubwa kutwaa Ubingwa wa Dunia hasa kwa vile wao ndio Timu yenye mafanikio makubwa Duniani.

Hata hivyo, Historia pia inaunga mkono kwa Timu ya Marekani ya Kusini kutwaa Kombe la Dunia kwani katika mara 4 zote Fainali za Kombe la Dunia kuchezwa Marekani ya Kusini Nchi za huko ndizo ziliibuka Mabingwa.

Ripoti hiyo inatabiri Brazil watatinga Fainali kwa kuzitoa Netherlands, Uruguay na Germany kwenye Raundi za Mtoano wakati Argentina itazibwaga Ecuador, Portugal na Spain.

No comments:

Post a Comment