Mwanamke aliyekuwa kinara wa mtandao uliokuwa unawaingiza watoto wadogo katika biashara ya ngono amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela nchini Uingereza.Inaarifiwa Amanda Spencer, alifanya urafiki na wasichana hao wadogo wengine wakiwa na umri wa miaka 13 kabla ya kuwalazimisha kufanya ngono na wanaume na kisha kuwalipa.
Mahakama ya Shefield iliambiwa kuwa Amanda alitumia pesa zake kwa madawa ya kulevya na pombe.Spenser mwenye umri wa miaka 23, alipatikana na hatia wiki jana kwa makosa 16 yote yakihusishwa na biashara ya ngono kwa watoto wadogo.Hata hivyo mahakama ilifutilia mbali makosa mengine 7 dhidi yake ikiwemo, kupanga na kufanikisha biashara ya ngono miongoni mwa watoto, kuwalazimisha watoto kuwa makahaba na kuwatumia vibaya watoto.Wakati wa kesi hiyo, mahakama iliarifiwa kuwa Spencer aliwalenga watoto ambao walikuwa hawana uwezo.Lakini Spencer alikana mashitaka yote dhidi yake akisema kuwa waathiriwa walisema uongo na kwamba hajawahi kukutana nao wala hawafahamu.Alishitakiwa pamoja na wanaume wengine wanne, lakini watatu waliachiliwa huku mshitakiwa mwenza mwenye umri wa miaka 68 Ian Foster akipatikana na hatia.
No comments:
Post a Comment