Usiku wa April 13 2014 lililipuka bomu kwenye baa moja Mianzini
Arusha na kujeruhi zaidi ya watu 15 wengi wao wakiwa wanatazama mpira
ambapo mpaka sasa haijajulikana ni nani alihusika.Usiku wa May 5 2014 yani jana saa mbili na dakika 20 umetokea mlipuko
mwingine ndani ya kanisa la KKKT Makongoro wilayani Ilemela Mwanza
ambao umethibitishwa na Polisi.
Polisi imethibitisha kwamba uchunguzi wa awali umeonyesha bomu hilo
ni la kienyeji na baada ya kulipuka limemuathiri mtu mmoja aitwae
Bernadetha Alfred kabila Mnyaturu mwenye umri wa miaka 25 ambae kwa sasa
anatibiwa kwenye hospitali ya Bugando.Jeshi la polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama bado wanaendelea
kuchunguza hili tukio manake hata aliefanya shambulio hili pia bado
hajajulikana.
Tuesday, 6 May 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment