Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuanzia msimu wa 2015/2016 itakuwa na timu 16 badala ya 14 za sasa.Mabadiliko hayo yamepitishwa na Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana
jana (Mei 3 mwaka huu) jijini Dar es Salaam baada ya kupokea mapendekezo
ya kuongeza idadi ya timu kutoka kwenye Kamati ya Mashindano.Uamuzi huo umefanywa kwa lengo la
kuongeza ushindani katika ligi hiyo, na kuwezesha wachezaji kupata mechi
nyingi zaidi za mashindano.
Kwa mabadiliko hayo maana yake ni kuwa Ligi
ya msimu wa 2015/2016 itakuwa na mechi 240 wakati kwa sasa ina mechi
182.Kuhusu idadi ya wachezaji wa kigeni
kwenye VPL, Kamati ya Utendaji itafanyia uamuzi mapendekezo katika eneo
hilo baada ya kwanza kupata maoni ya klabu za VPL na Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) ambazo Mei 11 mwaka huu zitakutana na Rais wa TFF, Jamal
Malinzi.Mapendekezo ya Kamati ya Mashindano ni
kuwa idadi ya wachezaji wa kigeni iendelee kuwa watano kama ilivyo
katika kanuni za sasa za VPL.
MTAALAMU WA NYASI BANDIA AWASILI
Mtaalamu wa nyasi bandia kutoka
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ian McClemen amewasili
nchini leo alfajiri (Mei 4 mwaka huu) ambapo atakuwepo kwa siku tatu.McClemen ameondoka leo (Mei 4 mwak huu)
kwenda Bukoba ambapo atakagua Uwanja wa Kaitaba, na kesho (Mei 5 mwaka
huu) atakwenda jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana.Viwanja hivyo vinawekwa nyasi bandia kwa
ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. Baada ya
ukaguzi huo, McClemen atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo
liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi
bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es
Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo
Pemba.
No comments:
Post a Comment