Majeshi ya usalama ya Nigeria yamewakamata watu kadha
katika mji mkuu wa nchi hiyo Abuja kufuatia mashambulio ya mabomu ya
hivi karibuni, zikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa Mkutano wa
Uchumi wa Dunia mjini humo.Wengi waliokamatwa wanasemekana kuwa raia wa kigeni, lakini hakuna taarifa zaidi za kina zilizotolewa.
Maafisa wameagiza kufungwa shule na ofisi za serikali wakati wa
mkutano huo, ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na marais wa Rwanda, Senegal
na Kenya pamoja na waziri mkuu wa China Li Keqiang.Serikali iko katika shinikizo kubwa la kukabiliana na kusambaa kwa ghasia nchini Nigeria.
Mlipuko wa Alhamisi uliua watu 19, wiki mbili baada ya mlipuko eneo la karibu na hapo kuua watu 75.
Hakuna kikundi kilichodai kuhusika na
mashambulio hayo, lakini wapiganaji wa Kiislam wa kundi la Boko Haram
wanatuhumiwa kuhusika na matukio hayo.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Nigeria amesema waliokamatwa Jumamosi wanahojiwa na wametoa "taarifa muhimu."Boko Haram pia wanaaminika kuhusika na utekaji
wa zaidi ya wanafunzi wa kike 200 kutoka shule yao katika jimbo la Borno
kaskazini mashariki mwa Nigeria zaidi ya wiki mbili zilizopita.Rais Goodluck Jonathan anatarajiwa kulihutubia
taifa Jumapili baada ya kukosolewa kwake namna anavyowashughulikia
wapiganaji wa Kiislam.Jumamosi serikali ya Marekani iliwaonya raia
kuhusu kuwepo mpango wa kushambuliwa kwa moja ya hoteli za Sheraton
karibu na Lagos, mji mkuu wa kibiashara wa Nigeria.
Sunday, 4 May 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment