Serikali ya Afghanistan imetangaza siku moja ya
maombolezo ya kitaifa kwa mamia ya watu waliofukiwa katika kifusi cha
udongo wakati maporomoko ya ardhi yalipokifukia kijiji chao Ijumaa.Gavana wa jimbo la Badakhshan, Shah Waliullah
Adib amesema kwamba kwa sasa hakuna matumaini ya kuwapata hai watu
zaidi ya 2,000 wanaoaminika kufukiwa katika nyumba zao.
Maafisa wa serikali walihitimisha rasmi Jumamosi shughuli za utafutaji wa watu walionusurika.Mashine za uchimbaji ziliondoka kijiji cha Ab Barik bila kutumika kutokana na eneo la tukio kutofikika kirahisi.
Sunday, 4 May 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment