Kiongozi wa waisilamu katika jimbo la Kano nchini Ngeria,Al-Haji Ado Bayero, amefariki.Kiongozi huyo mwenye kuheshimiwa sana miongoni mwa viongozi wengine wote nchini humo , amethibitishwa kufariki nchini humo.
Al-Haji Ado Bayero, alikuwa mtawala wa Kano tangu mwaka 1963 na alifariki baada ya kuugua kwa mda mrefu.Tangu wakati huo Nigeria imekabiliana na misukosuko ya mapinduzi ya kijeshi na ghasia zingine.
Alikuwa na umri wa miaka 84 na kutambuliwa kama
kiongozi wa muda mrefu sana na mkongwe zaidi wa waisilamu katika jimbo
hilo na pia alitambulika kama kiongozi wa pili mwenye ushaiwishi zaidi
kwa waisilamu Nigeria
Emir akiwa kwa Maombi katika jimbo la Kano
Marehemu Emir pia alitambuliwa kama kiongozi aliyependa amani.Miaka miwili iliyopita alinusurika kwa tundu la
sindano baada ya msafara wake kushambuliwa ambapo dereva wake na walinzi
wake wawili walifariki.Ilishukiwa kuwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu wenye itikadi kali, Boko Haram, ndio waliomshambulia.
Emir akiwa na mwanamfalme wa Uingereza Prince Charles
Boko Haram wamewashutumu viongozi wa kijadi
nchini Nigeria kwa kuwa vibaraka wa wanasiasa. Juma lililopita Emir wa
Gwoza aliuliwa na kundi hilo ambalo limetekeleza mashambulizi mengi
Kaskazini Mashariki mwa nnchi hiyo.Mwandishi wa BBC Sa'ad Abdullahi mjini Abuja
anasema kuwa emiralikuwa amerejea tu kutoka mjini London ambako alikuwa
anapokea matibabu.Maishani mwake alikuwa mfanyakazi wa banki, polisi, mbunge , balozi na mfanyabiashara maarufu.
No comments:
Post a Comment